Benki ya Kiislamu ya PBZ inaamini
kuwa huduma
inazotoa ambazo zinaenda na misingi ya Sharia
ya
Kiislamu ni kwa ajili ya watu wote waislamu na
wasiokua waislamu. Hali hii inapelekea
kuendelea
kuanzishwa kwa huduma nyingine zenye
kuleta
ushindani
wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Benki ya Kiislamu ya PBZ inasaidia
katika kujengana kukuza maadili ya jamii, kukuza ushirikiano wa jamii, na
kujenga utawala bora kwa kutoa hudumabila kujali itikadi/imani za kidini. Kwa
sasa Benki ya Kiislamu ya PBZ ina matawi matatu katika maeneo ya Ungujua, Pemba
na Dar es Salaam.
AL-MUDHARABAH
Akaunti ya Al-Mudharabah
Ni mkataba wa kibiashara wa kugawana
faida baina ya mtoaji fedha/mtaji (Rabbul Mal) na anaepokea fedha
(Mudharib) ambae ndiye anayefanya biashara. Katika mkataba wa Mudharabah, mteja
anayeweka fedha benki ndiye anakuwa mtoaji wa mtaji na Benki ya Kiislamu
ya PBZ ambayo inayopokea fedha za mteja na kuzifanyia biashara inakuwa
mjasiriamali kwa upande wa pili.
Makubaliano haya yanawezesha Mteja wa Benki ya Kiislamu ya PBZ kuingia ubia
katika kufanya biashara na faida inayopatika inagawanywa baina ya benki na
mteja katika kiwango wanachokubalina kabla.
Akauti ya Al-Mudharabaha
inamuwezesha mteja
- Kuingia ubia na benki katika kufanya biashara halali
kufuatana na misingi ya shariah ya Kiislamu.
- Kupata sehemu kubwa ya faida iliyohalali kutegemeana na
muda ambao fedha imewekwa.
- Mteja anaweza kuweka na kutoa fedha wakati wowote.
Aina za Akaunti ya Al-Mudharabah
Mteja anaweza kuweka fedha zake
katika Benki ya Kiislamu ya PBZ kwenye Akauti ya Al-Mudharabah zifuatazo
- Akanti ya Aiba ya Al-Mudharabah
- Akaunti ya Hundi ya Al-Mudharabah
- Akanti ya muda maalumu ya Al-Mudharabah
Sifa na faida ya Akaunti ya Akiba ya
Al-Mudharabah
- Kiwango cha kufungulia Akanti ni TZS 20,000
- Kiwango cha chini cha kubakiza katika Akanti ni TZS
10,000
- Akanti hii haitumii hundi
- Mteja naweza kutoa na kuweka fedha wakati wowote
- Mteja atalipwa faida ikiwa itapatikana katika kiwango
kilichokubalika kabla
- Mteja akiwa mtubinafsi atapatiwa kadi ya ATM ya Ikhalas
Sifa na faida ya Akaunti ya Hundi ya
Al-Mudharabah
- Akaunti hii inatumia hundi
- Kiwango cha kungulia Akanti kwa mtu binafsi ni TZS
200,000
- Kiwango cha chini cha kubakiza katika Akanti kwa mtu
binafsi ni TZS 100,000
- Kiwango cha kufungulia Akanti ya hundi ya
Al-Mudharabaha kwa Seriakli ni TZS 500,000
- Kiwango cha chini cha kubakiza katika Akaunti kwa
Serikali ni TZS. 250,000
- Kiwango cha kufungulia akaunti kwa kampuni ni TZS
300,000
- Kiwango cha chini cha kubakisha katika Akaunti kwa
Kampuni ni TZS 150,000
- Kiwango cha kufungulia Akaunti kwa taasisi zisizokua za
Kiserikali (NGO’s) ni TZS 100,000
- Kiwango cha chini cha kubakisha katika Akaunti kwa
tasisi zisizokua za Kiserikali ni TZS 50,000
- Fedha inayowekwa inaekezwa katika miradi inayokubalika
kufuata mising ya sheriah ya Kiislamu
- Mteja akiwa mtu binafsi atapatiwa kadi ya ATM – Ikhlas
Card
- Mteja anaeweka fedha nyingi kwa muda mrefu ndie
anaepata faida kubwa
- Mteja atalipwa faida kwa kiwango kilichokubalika.
Sifa na faida ya Akaunti ya Muda
Maalumu ya A-Mudharabah
- Mteja anaeweka fedha nyingi kwa muda mrefu ndie
anaepata faida kubwa
- Mteja atalipwa faida kwa kiwango tulichokubaliana
- Mteja hualikwa na kuelezwa juu ya miradi mbalimbali
inayohitajika kuwekezwa fedha na kuweza kuweka fedha zao
- Muda wa kuwekeza ni miezi 3, 6, 12 na 24
- Mteja huelezwa eneo au mradi ambao fedha zitaekezwa
- Kiwango cha chini cha kuweka ni TZS 1,000,000 kwa
kampuni na TZS 500,000 kwa watu binafsi.
- Faida inagawanywa kwa mujibu wa makubaliano yaliofikiwa
kabla.
Walengwa
- Watu wote Waislamu na wasiokua waislamu
- Wenye umri usiopungua miaka 18
- Wafanyabiashara
- Wakulima
- Wafanyakazi
- Serikali na Idara zake
- Mashirika ya Serikali
- Makampuni ya Watu binafsi
- Mashirika na taasisi zisizo za au ya Kiserikali
- Watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane (18)
wanaruhusiwa kufungua Akaunti chini ya udhamini wa mzazi au mlezi
| | |
|
No comments:
Post a Comment