FINANCING


Bai-Murahaba ni huduma inayomuwezesha mteja kukopa bidhaa na vifaa mbali mbali kwa ajili ya matumizi binafsi au biashara. Bai-Murabaha maana yake in mauziano ambayo yanajumuisha gharama na faida, na mkopaji hulazimika kulipa fedha taslimu siku ya mauziano au kulipa kwa mkupua mmoja au kwa vipingili siku za usoni.
Benki ya Kiislamu ya PBZ inatoa mkopo kwa njia ya Bia-Murabaha ikiwa ni mkataba wa kuuziana baina ya Muuzaji (Benki) na Mnunuzi (mkopaji) ambapo Benki inauza kwa Mkopaji bidhaa au vifaa kwa bei inayojumuisha gharama na faida. Mkopaji anapaswa kujua gharama ya bidhaa/vifaa pamoja na faida  iliyowekwa. Malipo ya mkopo huo yanafanyika katika muda wanaokubaliana baina ya Benki na mkopaji aidha kwa mkupuo mmoja au kwa vipingili sawa.



Sifa za Bia-Murabaha
  • Unaweza kukopa vifaa vya nyunbani
  • Unaweza kukopa vifaa nya ujenzi\Uvuvi, Usafiri  n.k.
  • Unaweza kukopa vifaa vya ofisini kama kompuyta, fanicha, n.k.
  • Mteja anaweza kukopa kitu chochote anachokitaka kulingana na sifa anazozitoa
  • Vifaa au vitu vinavyohusika ni vile vilivyohalalishwa katika Sheriah.
Faida
  • Kuepuka kulipa riba
  • Kukamilisha ndoto zako za kupata makazi mazuri naya kudumu kwa gharama nafuu
  • Kuweza kufanya biashara pasipo na mtaji kazi wakutosha
  • Unawaweka wateja wa Benki katika mazingira mazuri na kuondokana na umasikini.
Jinsi ya kupata huduma hii
Anaetaka huduma hii anapaswa
  • Awe ni mteja wa Benki ya Kiislamu ya PBZ kwa kiindi kisichopungua miezi sita (6)
  • Akiwa ni muajiriwa kuwe na mkataba baina ya Benki na Muajiri
  • Ikiwa Mteja ni Mfanyabiashara au Kampuni awasilishe:
    • Leseni ya Biashara
    • Usajili wa kulipa kodi (Tin na VRN)
    • Sehemu ya kufanyia biashara
    • Hesabu za biashara zisizopungua miaka miwili
    • Mtitiriko wa mapato na matumizi na jinsi atakavyoweza kulipa mkopo
    • Dhamana ya Mkopo
    • Taarifa nyengine yoyote inayohitajika.

No comments:

Post a Comment